Gazeti huru tz: Kitendo cha Heshima na Kishujaa Kilichofanywa na huyu Mwanajeshi wa USA wa Kwetu TZ Wangekiweza?

Wednesday, July 19, 2017

Kitendo cha Heshima na Kishujaa Kilichofanywa na huyu Mwanajeshi wa USA wa Kwetu TZ Wangekiweza?



Mwanadada mmoja wa Kimarekani aitwae Erin Hester aliyekuwa ndani ya Gari lake aliweza kumuona Mwanajeshi mmoja akifanya Kitendo ambacho ni adimu na nadra sana kukiona kwa Wanajeshi pale ambapo Mwanajeshi huyo aliweza kuonyesha kwamba kweli ' Uanajeshi ' ni zaidi ya ' Nidhamu ' ya kawaida ambayo unaweza kuikuta kwa Raia mwingine yoyote baada ya kuamua kushuka ghafla katika Gari lake tena katika ' Mataa ' huku Mvua kubwa sana ' ikinyesha ' na kuipigia ' Salute ' Gari ambayo ilikuwa imebeba ' Jeneza ' inakwenda ' Kuzika ' huku Yeye akiwa ameloana ' chapachapa '.

Na kilichowashangaza wengi ni kwamba hilo Gari lililobeba ' Jeneza ' lilikuwa ni la Raia tu halafu hata huyo ' Marehemu ' mwenyewe alikuwa hajulikani na huyu ' Askari ' mpiga ' Salute ' wala Ndugu wa ' Marehemu ' nao alikuwa hawajui kitu ambacho kiliwavutia ' Wamarekani ' wengi huko katika mji wa Kentucky na hatimaye kummiminia ' Kongole / Pongezi ' nyingi mno huyu Mwanajeshi / Mjeda.

Swali ni dogo tu je hii nidhamu ' iliyotukuka ' kutoka kwa huyu ' Afande ' wa Kimarekani tunaweza pia ' kuibahatisha ' siku moja kuiona kwa ' Wajeda ' wa Kitanzania hasa hasa katika matukio muhimu ya Gari zilizobeba ' Majeneza ' ya Raia huku ' Bogi / Mvua ' kubwa inanyesha?

Shikamooni ' Maafande / Wajeda ' wote nchini Tanzania hata wale mliopo sasa Sudan na Congo DR.



                              Weka Maoni Yako Hapa Chini

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. In sodales dapibus dui, sed iaculis metus facilisis sed. Etiam scelerisque molestie purus vel mollis Mauris.

No comments:

Post a Comment