Saturday, July 15, 2017
Unamtambuaje rafiki mwenye dalili za kuja kuwa adui
Rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi yakiwemo
• Kwenye mapenzi
• Kwenye biashara
• Kwenye kupata nafasi kazini
• Kwenye mahusiano na marafiki zenu
• Kwenye mikataba au tenda
Dalili/Mazingira
• Unasikia au unagundua anakusema vibaya kwa wengine, tofauti na akiwa na wewe
• Unahisi au unagundua anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani
• Unahisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako
• Unahisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni
Unafanyaje?
• Usimwamini sana mtu wa namna hii
• Usijiachilie na kuwa wazi sana kwa mtu huyu
• Pima ushauri wake na ikiwezekana uliza mtu mwingine pia.
Labels:
DARASA
No comments:
Post a Comment