Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza
imemaliza ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania na kueleza
kufurahishwa na namna Watanzania walivyoipokea timu hiyo.
Wayne Rooney (wa tatu kushoto) akiwa na wachezaji wenzake
walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu
ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam.
Timu ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo
juzi ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka
Kenya.
“Nimepata uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini
sasa Makamu wa Rais atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney
kupitia tovuti ya timu hiyo.
Pia katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru
mashabikji wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Great start to the pre-season. Special thanks to the fans
supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani za pekee
kwa Mashabiki wa Tanzania.
Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia
ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki
iliyooneshwa na mashabiki wa soka nchini.
Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas
wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza
kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye
mahitaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu
wa ngozi (Albino United).
Timu ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza
mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi,
Marais wastaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wageni mbalimbali
kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment